Home Habari za michezo AZAM COMPLEX KUANZIA SASA IITWE YANGA COMPLEX ALLY KAMWE AFUNGUA HAYA

AZAM COMPLEX KUANZIA SASA IITWE YANGA COMPLEX ALLY KAMWE AFUNGUA HAYA

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amewatupia dongo Klabu ya Azam baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Klabu ya Bahri ya nchini Ethiopia jana usiku kwa mikwaju ya penati.

Kamwe amedai kuwa kwa vile Uwanja wa Azam Complex unatumiwa na Yanga, basi ubadilishwe jina na kuitwa Yanga Complex Chamazi mpaka pale ambapo Yanga italerejea kutumia dimba la Mkapa ambalo linakarabitwa.

“Tunatuma maombi kwa TFF na Bodi ya Ligi ule uwanja ubadilishwe kuanzia sasa uitwe Yanga Complex. Tunakwenda kimataifa, tukiulizwa na CAF, Yanga ni timu, je, hii Azam ni nini? Tutajibu nini? Ni kiwanda au nini? Kwa hiyo tutaita Yanga Complex mpaka tutakapoondoka pale.

“Azam hakuna timu pale, kesho (leo) tukutane Yanga Complex Chamazi, anayebisha alete timu pale. Kesho (leo) tunakwenda kutambulisha Maxi Day pale na kuutambulisha rasmi ule kuwa uwanja wetu,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  MWENYE NAMBA KARUDI YANGA GAMONDI AKUNA KICHWA, KUFUMUA KIKOSI CAF