Home Uncategorized AZAM FC YAPANIA KUFANYA MAAJABU KWA WAETHIOPIA JUMAPILI

AZAM FC YAPANIA KUFANYA MAAJABU KWA WAETHIOPIA JUMAPILI


KIKOSI cha mabingwa wa kombe la Shirikisho Azam FC kimepania kufanya maajabu kwenye mchezo wao utakaochezwa Jumapili nchini Ethiopia dhidi ya Fasil Kenema.

SAzam FC kwa sasa ipo nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kwanza Agosti 11 kabla ya kurudiana na timu hiyo baada ya wiki mbili ndani ya jiji la Dar.

Jaffary Maganga, Ofisa Habari wa Azam FC, amesema kuwa kikosi kipo salama na mipango inakwenda kwa kasi.

“Kwa sasa kikosi cha kazi kipo Bahir Dar, Ethiopia Hoteli ya Solyana na tumewahi mapema ili kujiaanda na kile ambacho kimetuleta huku tuliko.

“Mchezo wetu kwa kimataifa ni mkubwa na mgumu ila imani yetu ni kupata matokeo chanya dhidi ya wapinzani wetu, kila kitu kinawezekana kikubwa sapoti na dua ya mashabiki,” amesema. 

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA