Home Uncategorized MABOSI MANCHESTER CITY WAKUBALIANA KUMPA NAMBA MPYA NYOTA WAO MPYA

MABOSI MANCHESTER CITY WAKUBALIANA KUMPA NAMBA MPYA NYOTA WAO MPYA


MABOSI wa Manchester City wamethibitisha kwamba nyota mpya aliyejiunga nao kwa ajili ya msimu ujao atatumia jezi namba 27.

Joao Cancelo amekamilisha usajili wake ndani ya kikosi cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England akitokea klabu ya Juventus kwa dau la pauni milioni 26.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ni pendekezo la Meneja Pep Guardiola na anakuwa mchezaji wa tatu kusaini.

Msimu uliopita akiwa ndani ya Juventus alitoa jumla ya assisti 5 na timu yake ilitwaa ubingwa wa Serie A pamoja na Italian Super Cup.

SOMA NA HII  KIONGOZI SIMBA AIOMBEA SAPOTI YANGA