Home Uncategorized NYONI SASA KUUNGANA NA WACHEZAJI WENZAKE BAADA YA MAPUMZIKO KUISHA

NYONI SASA KUUNGANA NA WACHEZAJI WENZAKE BAADA YA MAPUMZIKO KUISHA

BEKI mkongwe ndani ya Klabu ya Simba, Erasto Nyoni amesema kuwa anaamini kuwa atajumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya pamoja baada ya mapumziko ya mwezi mmoja kukamilika.

Nyoni alipata majeraha kwenye mchezo dhidi Yanga uliopigwa Uwanja wa Taifa Machi 8 ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona kwa muda wa mwezi mmoja.

“Nina amini kwamba baada ya muda wa mwezi mmoja nina amini nitaungana na wenzangu kwenye mazoezi, kikubwa ni kuomba Mungu tuwe salama kwani hili janga ni letu sote,” amesema.

SOMA NA HII  NDAYIRAGIJE ABEBA MATUMAINI YA WATANZANIA, APANIA KUFANYA MAAJABU MBELE YA KENYA