Home FA Cup BIASHARA UNITED YAIFUNGASHIA VIRAGO NAMUNGO KOMBE LA SHIRIKISHO

BIASHARA UNITED YAIFUNGASHIA VIRAGO NAMUNGO KOMBE LA SHIRIKISHO


BIASHARA United ya Mara inamsubiri mshindi wa mchezo wa kesho kati ya Mwadui v Yanga, unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kambarage.

Biashara United imeshakata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC. 

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Karume, Mara na watupiaji walikuwa ni Mpapi Nassib na Kalevin Friday ambaye alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti.

Yanga iliweka kambi Shinyanga kwa muda baada ya kumalizana na JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara na ilishinda mabao 2-0 Uwanja wa Jamhuri,Dodoma na jana, Mei 23 kiliwasilia Shinyanga kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

Bingwa mtetezi wa taji hilo ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes yeye atapambana na Dodoma Jiji, Mei 25, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  YANGA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO,