Home news KAGERA SUGAR KUANZA MAZOEZI LEO

KAGERA SUGAR KUANZA MAZOEZI LEO


 WAKATI Ligi Kuu Bara ikiwa imesimama kupisha michuano ya kombe la Azam Federation, Kocha Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Francis Baraza amesema timu yake imepanga kuanza mazoezi leo jumatatu baada ya kuwapa mapumziko wachezaji wake ya sikui 7.

 

Baraza ameliambia Championi Jumatatu kuwa “Baada ya ushindi kwenye mchezo wetu na Ruvu Shooting niliwapa wachezaji wangu mapumziko ya siku 7 ili wapumzishe miili yao kwa sababu walionekana kuchoka sana.

 “Lakini leo Jumatatu tunatarajia kuanza mazoezi kwa ajili ya kumalizia michezo mitano ya ligi ambayo imebaki mpaka sasa.

 

“Kiukweli najivunia namna ambavyo wachezaji wangu wamebadilika kiuchezaji kutokana na namna wanavyocheza na kuipatia timu matokeo maana nimeingiza vitu vingi kiufundi kwenye miili yao na wamepokea hivyo kwenye mazoezi yetu yanayoanza kesho (leo) tunakwenda kurekebisha makosa madogo. 

“Kabla ya ligi Mei 16 tumepanga kucheza jumla ya michezo 3 ya kirafiki ili wachezaji wangu wakae sawa maana katika ligi kuu kwa sasa ushindani ni mkubwa na tunachotaka sisi ni ushindi tu ili tukae sehemu salama na tumejipanga kuonyesha ushindani unaotakiwa ili tuweze kutimiza malengo ya kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo ili tuepuke janga la kushuka daraja” alisema Baraza.

 

 

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA LEO..NABI APANGA KUISHUSHA DARAJA MAZIMA MTIBWA SUGAR..."WANASUMBUA TIMU NYINGI SANA"...