Home Yanga SC YANGA YATAJA WACHEZAJI WA SIMBA WANAOSTAHILI KUCHEZA KLABU KUBWA ZAIDI

YANGA YATAJA WACHEZAJI WA SIMBA WANAOSTAHILI KUCHEZA KLABU KUBWA ZAIDI


UONGOZI wa Yanga umewataja wachezaji wa Simba ambao wanastahili kucheza timu kubwa zaidi kutokana na uwezo ambao wameuonyesha katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hiyo ni kutokana na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kutinga hatua ya robo fainali na kutolewa na Kaizer Chiefs kwa jumla ya mabao 4-3.

Katika mchezo wa kwanza waliocheza Uwanja wa FNB Soccer City Simba ilikubali kichapo cha mabao 4-0 na walikuja Uwanja wa Mkapa ngoma ilikuwa Simba 3-0 Kaizer Chiefs jambo ambalo limewafanya Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kimataifa kutolewa jumlajumla.

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, (CEO), Senzo Mbatha ambaye kwa sasa yupo ndani ya Yanga akiwa ni mshauri kuelekea mabadiliko amesema kuwa wachezaji wanastahili pongezi kwa walichokifanya huku wakiwa wanastahili pia kucheza katika klabu kubwa zaidi.

 Wachezaji aliowataja ni pamoja na beki wa kati Serge Wawa, kipa namba moja Aishi Manula, kiungo Clatous Chama, beki Shomari Kapombe na Luis Miquissone ambaye naye pia ni kiungo kwa kueleza kuwa wanastahili kucheza klabu kubwa zaidi.

Senzo amesema:”Heshima zote kwa wachezaji niliofanya nao kazi, ukitazama walichokifanya kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Manula, Wawa,Luis, Kapombe na Chama wanastahili timu kubwa zaidi,”. 

Naye Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz aliandika kwamba:”Kufuzu mchezo! Ila pongezi kwenu kwa kupambana kwa uwezo wenu wote ule ila nne zilikuwa nyingi,” .

SOMA NA HII  MASHINE YA KAZI ILIYOWAPA TABU SIMBA YAPANIA MAKUBWA NDANI YA YANGA