Home Uncategorized MWADUI FC: TUMEPATA TAABU SANA MSIMU HUU

MWADUI FC: TUMEPATA TAABU SANA MSIMU HUU

UONGOZI wa Mwadui FC umesema kuwa wachezaji wote walikuwa na wazo moja kichwani walipoingia uwanjani hali iliyowasaidia kupata matokeo chanya mbele ya wapinzani wao Geita FC mchezo wa Playoff uliochezwa uwanja wa Mwadui.

Akizungumza na Saleh Jembe, Katibu wa Mwadui, Ramadhan Kilao amesema kuwa ulikuwa ni mchezo wa jasho na damu na wachezaji waliambiwa ni lazmia watimize majukumu yao ipasavyo kwani nafasi yao ya mwisho ilikuwa nyumbani.

“Haikuwa rahisi, wachezaji wote wameajiriwa na kampuni ya Mwadui, sasa tulichowaambia ni kwamba walitakiwa kuongeza umakini na kutimiza majukumu yao ipasavyo kwani tulikuwa na nafasi moja mkononi tukiwa nyumbani.

“Tunajua kwamba wamepambana na walijitoa, pongezi wanastahili lakini ni majukumu yao kufanya hivyo, kwa sasa tumewaambia wameona taabu ambayo tumeipata msimu huu hivyo msimu ujao ni lazima kukaza mwanzo mwisho,”amesema.

SOMA NA HII  YANGA YAZIDIWA UJANJA KWA SIMBA YAPISHANA NA KIUNGO HUYU FUNDI WALIYEKUWA WAKIMPIGIA HESABU