Home Uncategorized KILICHOWABAKIZA NDANI YA TPL WABABE WA SIMBA CHATAJWA

KILICHOWABAKIZA NDANI YA TPL WABABE WA SIMBA CHATAJWA


KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa aliwaambia vijana wake watulie kwani mchezo ulikuwa mkononi mwao na kubaki kwenye ligi ilikuwa ni lazima hali iliyowafanya washinde mbele ya Pamba FC kwa mabao 2-0 mchezo wa Playoff.

Akizungumza na Salehe Jembe, Maxime amesema kuwa walijipanga kiasi cha kutosha kupata ushindi hali iliyowarahisishia njia ya kupenya.

“Tulicheza nao mchezo wa kwanza ugenini walikaza, haina maana kwamba Pamba sio timu nzuri hapana wapo vizuri ila nasi tupo vizuri pia ndio maana tumeshinda.

“Kwa sasa mipango ni mingi, hesabu kubwa ni kukisuka kikosi upya kitakacholeta ushindani msimu ujao maana mambo yalikuwa magumu kwetu mwisho wa siku tumeyamaliza,” amesema Maxime.

Kwa msimu wa 2018/19, Kagera Sugar wameweka rekodi ya kuifunga Simba ya Mbelgiji, Patrick Aussems nje ndani na kubeba jumla ya poini sita.

SOMA NA HII  CORONA YAVURUGAVURUGA MAMBO KIBAO YA ABDI BANDA