Home Uncategorized BREAKING:SENZO WA SIMBA AIBUKIA YANGA

BREAKING:SENZO WA SIMBA AIBUKIA YANGA

 

MUDA mfupi baada ya aliyekuwa  Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba , Senzo Mbatha leo Agosti 9 kutangaza kujiuzulu nafasi yake katika klabu hiyo, huku akiishushukuru klabu kwa mafanikio yaliyopatikana kwenye kipindi kifupi inaelezwa kuwa amepewa kazi ndani ya Yanga.


Ofisa Uhamasihaji wa Yanga, Antonio Nugaz alitupia tweet ya Senzo ambayo ilikuwa inaeleza kuwa amejiuzulu nafasi yake ndani ya Simba huku akiisindikiza na maneno kuwa anaimani atamuona hivi karibuni jambo lililozua mjadala.

Senzo ameonekana akiwa na wadau wa Yanga jambo ambalo limetoa tafsiri kwamba amepewa kazi ndani ya timu hiyo ya watani wa jadi.

Alipotafutwa Senzo ili aweze kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo simu yake ilikuwa haipatikani huku viongozi wa Yanga wakigoma kutolea ufafanuzi jambo hilo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ukurugenzi Simba, Mohamed Dewji amesema kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram:”Tumetoka mbali na bado safari inaendelea, tumepita mengi Wana Simbawenzangu. 

“Nawaomba WanaSimba wote mtulie. Simba ni kubwa kuliko mtu mmoja. Sisi viongozi tunawatumikia usiku na mchana bila kujali maslahi ya mtu binafsi bali Simba. Kazi inaendelea tuko imara,”

SOMA NA HII  LAMPARD ASHANGAZWA NA SILVA