Home Uncategorized MTIBWA SUGAR WAKIRI KUWA MSIMU WA 2019/20 ULIKUWA MBAYA KWAO

MTIBWA SUGAR WAKIRI KUWA MSIMU WA 2019/20 ULIKUWA MBAYA KWAO

 UONGOZI wa Mtibwa Sugar, umeweka bayana kuwa msimu wa 2019/20 ulikuwa ni mbaya kuliko misimu yote iliyotokea kwao ndani ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa hajawahi kushuhudia msimu mbaya kwa Mtibwa Sugar zaidi ya msimu ambao umekwisha.

“Tulikuwa na msimu mbayambayambaya kuliko yote ndani ya ligi tangu mwaka 1998 tupo ndani ya ligi na tulikuwa tukifanya vizuri ila kwa msimu wa 2019/20 mambo yalikuwa mabaya kiukweli.

“Tulikuwa kwenye hatari ya kushuka ila mwisho wa siku Mungu ametusaidia tumenusurika bado tupo hata msimu ujao tutaendelea kupambana, ila hatutausahau msimu uliopita.

“Tuna kikosi makini, wachezaji wanalipwa kwa wakati, maisha ni mazuri kambini ila ndio hivyo mpira una maajabu yake maisha yanaendelea,” amesema.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 38.

SOMA NA HII  ROLLERS YATUMIA POMBE KUJAZA UWANJA