Home Uncategorized BREAKING:KIBWANA SHOMARI ASAINI YANGA, ATAJWA KUWA MBADALA WA JUMA ABDUL

BREAKING:KIBWANA SHOMARI ASAINI YANGA, ATAJWA KUWA MBADALA WA JUMA ABDUL

 

KIBWANA Shomari, beki wa kulia wa Klabu ya Mtibwa Sugar leo ametangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam,


Kibwana anaingia kwenye usajili wa Yanga na kuwa nyota wa tano kusajiliwa baada ya dirisha la usajili kufunguliwa Agosti Mosi.

Wengine waliosajiliwa Yanga ni pamoja na Bakari Mwamnyeto beki kutoka Coastal Union, Abdalah Shaibu beki wa kati, Wazir Junior mshambuliaji kutoka Mbao FC, Yasin Mustapha beki kutoka Polisi Tanzania na Zawad Mauya kiungo kutoka Kagera Sugar.

Kibwana amesaini dili la miaka miwili anatajwa kuwa mbadala wa Juma Abdul ambaye mkataba wake umeisha Yanga na hajaongezewa baada ya kushindwana na mabosi wa Yanga.
SOMA NA HII  VIDEO: ALICHOKISEMA MUSONYE BAADA YA KUPATA MRITHI WAKE NDANI YA CECAFA