Home news BAADA YA KUTUPIA GENK MBAPPE WA BONGO AWEKA WAZI MIPANGO YAKE

BAADA YA KUTUPIA GENK MBAPPE WA BONGO AWEKA WAZI MIPANGO YAKE


BAADA ya juzi Jumatatu kufanikiwa kutupia bao lake la pili ndani ya kikosi cha klabu ya Genk, mshambuliaji kinda wa kimataifa wa Tanzania, Kelvin John ‘Mbappe’ ametamba kuwa malengo yake ni kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya wakubwa ya Genk.

Mbappe alijiunga na kutangazwa rasmi na Genk Julai 25, mwaka huu kwa mkataba wa miaka mitatu ambao utamuweka ndani ya timu hiyo mpaka mwaka 2024, huku ikielezwa kuwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alikuwa sehemu kubwa ya ushawishi wa usajili huo.

Katika michezo miwili iliyopita nyota huyo amefanikiwa kuifungia KRC Genk ya vijana mabao mawili.

Akizungumzia mipango yake, Mbappe amesema: “Najisikia furaha kuwa sehemu ya kikosi cha klabu ya Genk, nashukuru kwa ushirikiano ambao nimekuwa nikiupata kutoka kwa wenzangu ambao ni wazi umenifanya nizoee mazingira mapema, na kufanya vizuri katika michezo miwili iliyopita.

“Malengo yangu ni kuhakikisha najitahidi kuonyesha uwezo mkubwa ili niweze kumshawishi kocha aweze kunipa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya wakubwa.”

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUANZA KWA VIPIGO...MKENYA AIPELEKA SIMBA ROBO FAINAL CAF...AGUNA KUHUSU YANGA..