Home Uncategorized SINGIDA UNITED YAWATOA HOFU MASHABIKI WAO KUHUSU ISHU YA USAJILI KWA FURSA

SINGIDA UNITED YAWATOA HOFU MASHABIKI WAO KUHUSU ISHU YA USAJILI KWA FURSA

UONGOZI wa Singida United, umesama kuwa kufanya usajili kwa mtindo wa kipekee kwa kutoa fursa kwa wenye vipaji kujitokeza huku dozi yao ikiwa ni asubuhi na jioni haina maana kwamba hawatasajili kiufundi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa mashabiki wasiwe na hofu benchi la ufundi chini ya Felix Minziro wapo makini hivyo kutangaza fursa hiyo haina maana kwamba hawatafanya usajili wa maana. 

“Kufanya majaribio kwa wachezaji haina maana kwamba hatutafanya usajili, tupo makini na usajili na tutafanya kazi yetu kimyakimya, 

“Cha msingi ni wachezaji kutambua kwamba muda wa majaribio dozi itakuwa ni asubuhi na jioni hivyo wakati wao ni sasa cha kuwakumbusha tu gharama zote ni juu yao zoezi litaanza tarehe 12 mpaka 16 uwanja wetu wa Namfua,” amesema.

SOMA NA HII  NYOTA MWINGINE, MTAMBO WA MABAO NDANI YA YANGA HATIHATI KUIKOSA SIMBA JULAI 12