Home Uncategorized CHELSEA YAKUBALI KUMUACHIA NYOTA WAO LUZ KWA HASARA KUTUA ARSENAL

CHELSEA YAKUBALI KUMUACHIA NYOTA WAO LUZ KWA HASARA KUTUA ARSENAL


ARSENAL inatakiwa ivunje kibubu na kuweka mezani dau la pauni milioni 12 Kwa Chelsea ili kumpata nyota David Luiz.

Beki huyo raia wa Brazil amewaambia mabosi wake kuwa anataka kusepa ndani ya kikosi hicho na bosi mpya Frank Lampard akamwambia haina noma waweza kusepa.

Chelsea ilimnasa nyota huyo mwaka 2016 kwa dau la pauni milioni 32 wamekubali dau dogo ili kupata mchezaji nje ya klabu yao.

Luiz amebakiza mwaka mmoja pekee ndani ya Stamford Bridge hivyo Lampard anajipanga kuipokea hasara hiyo iwapo nyota huyo atasepa.

SOMA NA HII  OHOO KUMBE SKUDU ANAJAMBO LAKE NA GAMONDI...... ISHU NZIMA IKO HIVI