Home Habari za michezo BILIONI 20 ZA MO DEWJI SIMBA ZATENGWA KAMA BAJETI YA MISHAHARA YANGA...

BILIONI 20 ZA MO DEWJI SIMBA ZATENGWA KAMA BAJETI YA MISHAHARA YANGA KWA MSIMU UJOA..

Habari za Yanga leo

Wakati Rais wa Heshima Simba Mo Dewji aliwekeza kwa kununua hisa za Bilioni 20 za timu hiyo, watani zao Klabu ya Yanga imetenga bajeti ya Sh20.8 bilioni kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano mbalimbali ya ndani na ya kimataifa.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa klabu hiyo Mkurugenzi wa Fedha, Sabri Sadick amesema ana amini kupitia bajeti hiyo italeta tija kwao msimu ujao na kuweza kufanya vizuri zaidi.

“Katika vyanzo vya mapato tuna Sh14.8 bilioni hivyo tuna upungufu wa Sh6 bilioni ambazo tunaamini tutafanyia kazi kwa haraka iwezekanavyo kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali ili kufikia malengo tuliyojiwekea.”

Aidha Sabri aliongeza kiasi hicho ni zaidi ya msimu uliopita kwani timu hiyo ilitumia Sh17.8 bilioni huku matumizi kwa msimu mzima yakiwa ni Sh17.3 bilioni.

“Hadi sasa kiasi cha fedha zilizobaki kwa msimu uliomalizika ni Sh581 milioni, hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa ili kuongeza ufanisi zaidi kwa timu yetu msimu ujao,”amesema.

Katika matumizi ya msimu uliopita Sabri amesema fedha hizo zimetokana na udhamini, kiingilio cha milangoni, ada za wanachama, zawadi ya ushindi, mauzo ya wachezaji, faida ya jezi, mikopo na mapato mengine.

Yanga Inafanya mkutano wake mkuu jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) ikiwa ni wa kwanza tangu uwaingize madarakani Rais wa klabu hiyo, Hersi Said, Makamu wa Rais, Arafat Haji na wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa Julai mwaka jana.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSAINI TU ...'SURE BOY' APEWA JEZI YENYE GUNDU ..KILA ALIYEIVAA HAKUDUMU NA YANGA..