Home news KIKOSI CHA SIMBA KUREJEA LEO DAR

KIKOSI CHA SIMBA KUREJEA LEO DAR


 IMEELEZWA kuwa baada ya kambi ya muda wa wiki mbili ndani ya Jiji la Utalii Tanzania, Arusha kikosi cha Simba kinatarajia kurejea leo Dar.

Chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes kikosi hicho kiliweza kucheza mechi tatu za kirafiki ikiwa ni lengo la kujiweka sawa.

Ilikuwa namna hii Simba 1-1 Coastal Union, Simba 1-0 Fountain Gate na Simba 2-1 Aigle Noir ya Burundi.

Kikosi hicho kinarejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye tamasha la Simba Day ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.


SOMA NA HII  HILI HAPA 'KOSI' LA MNYAMA DHIDI YA AZAM...SAKHO TARATIIBU ANAKUJA..WAWA NA BOCCO MHHH....