Home Ligi Kuu RUVU SHOOTING YATEMBEZA 5G BONGO

RUVU SHOOTING YATEMBEZA 5G BONGO


KIKOSI cha Ruvu Shooting kinachonolewa na Kocha Mkuu, Charles Mkwasa kimewashushia kichapo cha mabao 5-1Mwadui FC na kuzidi kuzamisha matumaini ya timu hiyo kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.


Ni Edward Manyama alifungua pazi la mabao dakika ya 17 na Shaban Msalla akapachika mabao mawili ilikuwa dakika ya 37 na 82, Richard yeye alipachika moja dakika ya 48 sawa  na Abrahaman Mussa aliyepachila bao dakika ya 76.


Bao pekee la Mwadui FC lilipachikwa na Mohamed Hashim dakika ya 57 ilikuwa Uwanja Mabatini yalipo maskani ya Ruvu Shooting. 


Ushindi huo unaifanya Ruvu Shooting kufikisha jumla ya pointi 37 ikiwa nafasi ya 6 huku Mwadui ikibaki na pointi 16 nafasi ya 18 kwenye msimamo

SOMA NA HII  STRAIKA WA SIMBA AIPA JEURI KMC