Home news RAJA CASABLANCA YAWASHUKURU WATANZANIA

RAJA CASABLANCA YAWASHUKURU WATANZANIA

 


BAADA ya Klabu ya Raja Casablanca ya Morocco kusepa na pointi tatu mbele ya Namungo FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, timu hiyo imewashukuru Watanzania kwa ukarimu wao.

Mchezo huo uliochezwa jana Aprili,21 Uwanja wa Mkapa Namungo ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Seleman iliokota mabao matatu nyavuni huku lango la wapinzani likiwa salama dakika zote 90.

Ni Illias Haddad alipachika bao dakika ya 9, Fabrice Ngoma alipachika la pili dakika ya 14 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Zakaria Habti dakika ya 36.

Mohamed Bekkari, Kocha  wa Raja Casablanca amesema kuwa anafurahi kuwa Tanzania na namna ambavyo watu wake wamekuwa ni wakarimu.

Akizungumza jana, Bekkari amesema kuwa wanafurahi kwa kuwa wampeta pointi tatu pamoja na huduma nzuri walizopata baada ya kuwa Tanzania.

“Imekuwa furaha kwetu kupata pointi tatu na hatujapoteza mchezo, kikubwa ni furaha na tunawashukuru Watanzania kwa sapoti yao pamoja na ukarimu,” .

Katika kundi D kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho,  Raja Casablanca inaongoza kundi ikiwa na pointi 15 baada ya kushinda mechi zote tano na Namungo ipo nafasi ya 4 ikiwa haijakusanya pointi. 

SOMA NA HII  DAKTARI WA VIUNGO YANGA AKOMAA NA MAXI ISHU IKO HIVI