Home epl HUYU HAPA ATAJWA KUWA MRITHI WA JOSE MOURINHO

HUYU HAPA ATAJWA KUWA MRITHI WA JOSE MOURINHO

 


IMEELEZWA kuwa Julien Nagelsmann ambaye ni Kocha Mkuu wa Klabu ya RB Leipzig atapewa mikoba ya Jose Mourinho ambaye amefutwa kazi ndani ya Klabu ya Tottenham Hotspurs.

Spurs baada ya kumfuta kazi Mourinho kutokana  na kushindwa kuwa na mwendo mzuri ipo chini ya Ryna Mason mwenye miaka 29 ambaye anatoka katika Akadem ya Tottenham atafanya kazi hiyo mpaka Kocha mpya atakapopatikana.

Kocha huyo ndani ya kikosi hicho cha Leipzing mkataba wake unadumu mpaka Juni 2023 hivyo mabosi wa Spurs wana kazi ya kuvunja mkataba wake ili kuipata saini yake.

Mourinho alifutwa kazi baada ya kucheza jumla ya mechi sita mfululizo bila ya kuwa na mwendo mzuri ambapo aliambulia ushindi mechi moja na aliondolewa kwenye Europa League, kwenye FA licha ya kwamba aliifikisha timu hiyo Carabao Cup hatua ya fainali.

Dau lake ambalo linatajwa kwa kocha huyo ambaye ataifundisha Spurs ni pauni milioni 10 pia hata Bayern Munich nao wanampigia hesabu.

SOMA NA HII  SUAREZ 'AMCHANA' KOEMAN