Home kimataifa SUAREZ ‘AMCHANA’ KOEMAN

SUAREZ ‘AMCHANA’ KOEMAN


 STAA wa Klabu ya Atletico Madrid, Luis Suarez amemtupia dongo la maana Kocha Mkuu wa Klabu ya Barcelona, Ronald Koeman kwamba hana utu katika masuala ya kazi yake.

Raia huyo wa Uruguay msimu uliopita aliruhusiwa kujiunga na Atletico Madrid kwa pauni milioni 5.5 akitokea Klabu ya Barcelona baada ya kupigiwa simu na Koeman kwa muda wa sekunde kadhaa kisha akaambiwa hahitajiki ndani ya timu hiyo ya Barcelona aliyokuwa akiitumikia.

Suarez ambaye walipokutana na Barcelona hivi karibuni kwenye mchezo wa La Liga aliwatungua bao moja na hakushangilia kwenye ushindi wa mabao 2-0 bado kitendo hicho kinaishi kwenye akili yake.

Nyota huyo amebainisha kwamba kitendo cha Koeman kutumia sekundi 40 kwenye simu kilimuumiza na hata alipwatungua Uwanja wa Wanda Metropolitano bado kuna jambo lilikuwa linazunguka kichwani mwake.

“Simu ya Koeman kuniambia kwamba hanitaki ilidumu kwa sekunde 40 tu, siyo sahihi na sio njia sahihi ya kuachana na mchezaji mkubwa,”. 

SOMA NA HII  BARCELONA HALI TETE KIUCHUMI...WACHEZAJI WAGOMA...WANATAKA MISHAHARA YAO