Home CAF SIMBA WAIPONZA RS BERKANE…CAF WAFANYA MAAMUZI MAGUMU…WATAKIWA KULIPA MILION 200..

SIMBA WAIPONZA RS BERKANE…CAF WAFANYA MAAMUZI MAGUMU…WATAKIWA KULIPA MILION 200..


Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Afrika, CAF imetoa adhabu kwa Klabu ya RS Berkane katika mechi mbili za Kombe ka Shirikisho Afrika dhidi ya Simba ule wa awali uliochezwa Morocco pamoja na ule wa pili uliochezwa Dar.

Taarifa iliyotolewa na CAF leo imeeleza kuwa kwenye mchezo wa RS Berkane dhidi ya Simba uliochezwa Februari 27, 2022 CAF imewapiga RS Berkane faini ya Dola za Marekani 8000 baada ya mashabiki wa timu kufanya vurugu na kutupa vitu kwenye eneo la kuchezea (pitch).

Pia kwenye mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba 1-0 RS Berkane kiongozi wa RS Berkane la Mr Madrane aliweza kuingia kwenye sehemu ya kuchezea na kuwashawishi wachezaji pamoja na benchi la ufundi kuungana naye kupinga hali hiyo huku akionekana kupinga maamuzi ya refa jambo lililopelekea mchezo kusimama kwa muda wa dakika 5.

CAF imemsimamisha Majid Madrane kwa muda wa miezi 12 kutojihusisha na masuala ya michezo yanayohusiana na CAF na Klabu ya RS Berkane imepigwa faini ya USD 100,000 sawa na zaidi ya Tsh milioni 200 kutokana na tabia ya M.Madrane.

SOMA NA HII  KUHUSU YANGA KUSHIRIKI 'AFL' MSIMU HUU....CAF WAIPA JIBU HILI YANGA...ENG HERSI ATIA UZITO..