Home Habari za michezo KUHUSU ILE ISHU YA FEI TOTO KUIPIGA CHINI YANGA…ALLY KAMWE LEO KAIBUKA...

KUHUSU ILE ISHU YA FEI TOTO KUIPIGA CHINI YANGA…ALLY KAMWE LEO KAIBUKA NA HILI JIPYA…

Habari za Yanga SC

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa hakuwahi kuamini iwapo aliyekuwa kiungo wa klabu hiyo, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ angeondoka klabuni hapo.

Kamwe amesema hayo kupitia Documentary ya Yanga iliyozinduliwa juzi huku akibainisha kuwa, tayari alikuwa ameshazungumza nae na kumpa mbinu nzuri ya kutatua jambo lake na uongozi wa klabu kabla ya kufanya maamuzi hayo.

“Sikuwahi kuamini kama Feitoto ataondoka Yanga kwa sababu suala lake la kutaka kuondoka aliwahi kuniambia, tukashauriana na mimi nikampa njia nzuri sana ya kupita.

“Ukiachana na mpira Feitoto kwangu ni rafiki, wakati tupo Sudan tukijiandaa kucheza dhidi ya Al Hilal tukiwa tunapiga story na Feitoto aliniambia anataka kuondoka.

“Alisema haoni kama anapewa thamani anayostahili ukilinganisha na anachotoa. Nikamwambia asiondoke lakini afanye vizuri zaidi halafu awafate viongozi kuomba kuboreshewa maslahi yake.

“Tukakubaliana msimu wa 2022|23 atafunga magoli zaidi ya 10 na assists kuanzia nane lakini yeye akasema atafunga magoli 13 na atatoa assists nane.

“Baada ya mazungumzo yale mimi nikaandika habari nikaichapicha Yanga App kwamba malengo ya Feitoto msimu huu ni kufunga magoli 13 na kutoa assists nane ” – Ally Kamwe kupitia Yanga Documentary.

Feitoto aliingia kwenye mgogoro na klabu yake jambo lililopelekea Rais Samia Suluhu kuingilia kati, hali iliyowalazimu viongozi wa Yanga kumuuza katika klabu ya Azam.

SOMA NA HII  KISA RAFU ZA AUCHO.....MANARA 'AMTOA NGEU YA USO' JEMEDARI SAIDI...