Home Habari za michezo KISA RAFU ZA AUCHO…..MANARA ‘AMTOA NGEU YA USO’ JEMEDARI SAIDI…

KISA RAFU ZA AUCHO…..MANARA ‘AMTOA NGEU YA USO’ JEMEDARI SAIDI…

Habari za Yanga

Baada ya baadhi ya wachambuzi wa soka Tanzania akiwemo Jemedari Said kumtaja kiungo wa Yanga SC, Khalid Aucho kuwa anaongoza kwa kucheza rafu, aliyekuwa mhamasishaji wa timu hiyo, Haji Manara ameibuka na kuwavaa wachambuzi hao.

Manara amesema wachambuzi wengi hivi ssa wanakosa uhalali wa kukosoa kutokana na kuwa na ubaguzi katika chambuzi zao.

Hii inatokana na kauli ya Jemedari kuwa, Aucho alitakiwa kupewa kadi nyekundu kipindi cha kwanza kwenye mchezo wao wa weekend iliyopita dhidi ya KMC, katika Dimba la Jamhuri Dodoma.

“Hawa wakikosoa sema na wale wakikosoa sema pia. Hawa hawajui chochote katika mpira. Mchezaji katimbwa. Ngoja nimwambie Aucho kazi ya kucheza tumuachie yeye, lakini kazi ya kupambana na hawa wachambuzi watuachie sisi.

“Sisi tutapambana na hawa wachambuzi maana ndiyo kazi yetu. Hii sio kazi yake, ni kazi yetu. Kwanza hawa wachambuzi wenyewe wote wamenikuta,“ amesema Haji.

SOMA NA HII  HUKO CAF NI YANGA NABI SAHANI MOJA LIGI YA MABINGWA