Home Habari za michezo KUHUSU NANI BORA KATI YA GAMONDI NA NABI…EDO KUMWEMBE KAANIKA CHAGUO LAKE…

KUHUSU NANI BORA KATI YA GAMONDI NA NABI…EDO KUMWEMBE KAANIKA CHAGUO LAKE…

Habari za Yanga leo

Baada ya wengi kuwa na mashaka na kiwango cha Yanga kwa siku za karibuni walianza kuweka mashaka katika mbinu za Mwalimu Miguel Gamondi.

Mchambuzi wa michezo kutoka Wasafi FM, Edo Kumwembe anasema;

“Kuna jambo la kujiuliza kuhusu ubora wa kocha aliyepita, Nasireddine Nabi na kocha wa sasa Miguel Gamondi. Ngumu kujua tofauti yao kwa namna Yanga inavyocheza. Kuna watu wamekuwa na wasiwasi na Gamondi baada ya hivi karibuni Yanga kusuasua katika ufungaji.Hata hivyo ukifuatilia namba unaweza kuona kuwa Gamondi anaweza kuwa bora kuliko Nabi mpaka sasa. Tunapaswa kusubiri na kuona mpaka mwishoni nani ataibuka mbabe.”

Kocha Miguel Gamondi alitua nchini mwanzoni mwa msimu huu ambapo moja ya matukio kumbukwa akiwa na timu yake ni kuifunga Simba iliyotimia jumla ya magoli 5-1.

Hata hivyo, Gamondi ambaye pia si mgeni na soka la Afrika anasifiwa kwa kuibadilisha Yanga na kuifanya icheze soka la kasi zaidi na la kuvutia kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Nabi.

Yanga kesho kutwa watakuwa na kibarua kigumu mbele yao kwa kutafuta ushindi mbele ya waarabu mchezo utakaochezwa kwenye dimba ya Mkapa .

Yanga ikifanikiwa kupata ushindi katika mchezo huo itakuwa imejiwekea nafasi kubwa ya kufuzu kwenda hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msimu uliopita Yanga walifika Fainal ya michuano ya kombe la Shirikisho chini ya Nabi rekodi ambayo ni mpya kwa miaka ya hivi karibuni kufikiwa na klabu za Tanzania.

SOMA NA HII  JICHOTEE MAPESA UTAKAVYO NA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET....!