Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MZIKI WA SIMBA ULIVYO….KOCHA WA ASEC KAGUNA WEE..KISHA AKASEMA...

BAADA YA KUONA MZIKI WA SIMBA ULIVYO….KOCHA WA ASEC KAGUNA WEE..KISHA AKASEMA HILI..

Habari za Michezo leo

Kocha wa Asec Mimosas, Juliet Chevalier, amesema mechi ijayo dhidi ya Simba inampa presha kutokana na hesabu zao lakini wanapigo la kumkosa mshambuliaji wao hatari Sankara Karamoko, mwenye rekodi za kufunga mabao manne katika mechi nne za michuano hiyo na saba katika ligi.

Lakini bado wamebakiwa na Serge Pokou aliyewafunga Simba mara ya mwisho Kwa Mkapa naye akiwa na rekodi ya kuwa na mabao manne katika ligi huku kimataifa akiwa nalo moja. Asec wana pointi 10 na tayari wameshafuzu robo fainali.

Safu ya ushambuliaji mpya ya Simba yenye pointi 5 kwenye nafasi ya pili, inabebwa na Freddy Kouablan mwenye bao moja na Pa Omary Jobe akiwa na mawili mpaka sasa, katika mechi tano walizocheza kila mmoja michuano ya ndani.

Akizungumza na Mwananchi, kocha huyo alisema, Simba itataka kushinda na watacheza mechi hiyo kama fainali yao wakati wao wanataka alama angalau mbili au tatu kwenye mechi zao mbili zilizosalia ili waongoze kundi hilo.

“Nilikuwa kwenye wiki mbili nzito za kuijenga upya safu yangu ya ushambuliaji bila Sankara Karamoko ambaye ameshauzwa katika usajili wa dirisha dogo.

“Wakati wapinzani wetu wako na watu na timu mpya tofauti na ile tuliyokutana nayo kabla hivyo haitakuwa mechi rahisi, tutakuwa katika uwanja wa nyumbani,”alisema kocha Juliet.

Asec inaongoza kundi B ikiwa na pointi 10 ikifuatiwa na Simba yenye tano, katika mechi nne za mwisho za ligi wameshinda mara mbili na zote wakiwa nyumbani, huku ugenini wakiwa wamepoteza michezo miwili, Rekodi za na Simba zinaonyesha kuwa kila wanapokutana nao katika uwanja wao hawajawahi kuwaacha salama.

Nako kwa Wekundu wa Msimbazi mambo yanajirudia kwani katika mechi mbili za mwisho walizocheza nao kwa Mkapa wamewafunga mabao 3-1 na kutoka na sare ya 1-1.

Kutokana na rekodi hizo za kutotoka salama ugenini, Simba wanaonekana kuwa na kazi ya ziada katika mechi hiyo itakayochezwa Ijumaa ya Februari 23 nchini Ivory Coast na wametumia muda mwingi kujiandaa huku wakiahirishiwa mechi dhidi ya Mtibwa.

Kundi B

Asec Mimosas – mechi 4, alama 10
Simba SC – mechi 4, alama 5
Jwaneng Galaxy – mechi 4, alama 4
Wydad Casablanca – mechi 4, alama 3.

SOMA NA HII  WAKATI WAKIJIANDAA NA WASAUZI KESHO KUTWA....SIMBA WAIPA YANGA SIKU 5 TU...AHMED ALLY AWANANGA..