Home Habari za michezo KUHUSU DILI LA KIPA MPYA SIMBA.. UKWELI WOTE A-Z HUU HAPA…

KUHUSU DILI LA KIPA MPYA SIMBA.. UKWELI WOTE A-Z HUU HAPA…

Tetesi za Usajili Simba

Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano ya kuinasa saini ya Mlinda Lango, Ayoub Lakred aliyekuwa akiichezea timu ya FAR Rabat ya nchini Morocco inayonolewa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Young Africans, Nasreddine Nabi.

Chanzo Makini kutoka ndani ya Simba SC kimeeleza kuwa, makubaliano ya pande hizo mbili yamefikiwa ikiwa ni siku chache tangu kuachana na Malinda Lango kutoka nchini Brazili, Jefferson Luis aliyeondolewa kambini nchini Uturuki kutokana na majeraha ya misuli.

“Ni kweli yupo nchini na maongezi hadi sasa yanaendelea vizuri, ni matumaini yetu atakuwa msaada mkubwa kutokana na ushiriki wetu wa mashindano mengi ya ndani na kimataifa,” kimeeleza chanzo hicho.

Lakred mwenye umri wa miaka 28, alichezea FAR Rabat, timu nyingine aliyowahi kuichezea ni RS Berkane.

Usajili wa Lakred unakuwa ni wa pili kwa Mlinda Lango ndani ya kikosi cha Simba SC.

SOMA NA HII  HUU HAPA 'UCHAWI' WA AZIZI KI KUWA MOTO MSIMU HUU NDANI YA YANGA....BALAA LAKE SIO POA..