Home Habari za michezo BAADA YA KUICHAPA KWA MBINDE SINGIDA JANA…AHMED ALLY KAJA NA HILI JIPYA...

BAADA YA KUICHAPA KWA MBINDE SINGIDA JANA…AHMED ALLY KAJA NA HILI JIPYA KWA SIMBA…

Habari za Simba leo

Meneja wa Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally amesema wanaami mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans hautakuwa mgumu, kama ilivyokuwa kwa Singida Fountain Gate ambayo wameitoa kwa changamoto ya Mikwaju ya Peneti.

Simba SC ilipata wakati mgumu katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate jana Alhamis (Agosti 10), na kujikuta ikisonga mbele kwa changamoto ya Mikwaju ya Penati 4-2, baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Ahmed Ally amesema kabla ya mchezo huo kupigwa Uwanja wa CCM Mkwakwani alitabiri mambo yangekuwa magumu na ndivyo ilivyokuwa, kutokana na ubora wa kikosi cha Singida Fountain Gate.

“Tulisema mechi yetu ngumu katika mashindano haya ni hawa Singida Fountaine Gate. Unaweza kuwachukuia poa Singida Fountain Gate kwa uchanga wa jina lao lakini wana ubora mkubwa kiwanjani.”

“Tuliamini mechi yetu na wao itakuwa ngumu, na ilikuwa hivyo, hadi kufikia hatua ya matuta na tumefanikiwa kuvuka, tunapokwenda ni kutafuna tu.”

“Tulikuwa tunaitaka hii Fainali, kimsingi tumekuja Tanga kwa ajili ya mechi hii na huu ni mwaka wetu” amesema Ahmed Ally

Simba SC itacheza Fainali dhidi ya Young Africans Jumapili (Agosti 13), katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, mchezo ambao utatanguliwa na ule wa kumsaka mshindi wa tatu kati ya Singida Fountain Gate dhidi ya Azam FC.

SOMA NA HII  KIKOSI RASMI CHA AZAM FC 2021/22 HIKI HAPA