Home Habari za michezo KUHUSU MGOLI ALIOUFUNGA KWA AZAM…AZIZI KI AFICHUA YA NYUMA YA PAZIA…

KUHUSU MGOLI ALIOUFUNGA KWA AZAM…AZIZI KI AFICHUA YA NYUMA YA PAZIA…

Habari za Yanga SC

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burkina Faso Stephen Aziz Ki, ametoboa siri kwa kusema Kocha Mkuu wa Young Africans Miguel Angel Gamondi alimpa maelekezo maalum kabla hajaingia uwanjani kuikabili Azam FC.

Young Africans juzi Jumatano (Agosti 09) iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii uliofanyika Uwanja wa CCM Mkwakwani, jijini Tanga.

Aziz Ki amesema Kocha Gamondi alimpa maelekezo ambayo aliyafanyia kazi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha anaisaidia timu kupata ushindi.

Amesema mchezo huo haukuwa rahisi na iliwachukua Young Africans hadi katika dakika za mwisho kupata matokeo, kitu ambacho walifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Nilipewa maelekezo maalumu na Kocha Gamondi, kwani kabla ya kuingia nilizungumza naye kwa muda.

“Tulilazimika kubadilisha mchezo na kuhakikisha tunapata ushindi, mchezo haukuwa rahisi kwa pande zote, kwani kila timu imefanya usajili wa kuhakikisha msimu mpya unakuwa tishio” amesema

Young Africans itacheza Fainali Jumapili (Agosti 13) dhidi ya Simba SC iliyotoa Singida Fountain Gate kwa changamoto ya mikwaju ya Penati 4-2 jana Alhamis (Agosti 10) katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.

SOMA NA HII  SHABIKI:- KAMA SIO SERIKALI....MANGUNGU TUNGEMTUNDIKA MLIMA KILIMANJARO...