Home Uncategorized AUSSEMS AIBUKA TENA, ATOA TAMKO JUU YA SIMBA

AUSSEMS AIBUKA TENA, ATOA TAMKO JUU YA SIMBA


KOCHA wa zamani wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa amesikia kelele za mashabiki wa timu hiyo wakishinikiza uongozi umrudishe kufundisha timu hiyo lakini kwa upande wake hafikirii kurejea nchini Tanzania kwa kuwa ni wakati wa kuvuna walichopanda awali.

Aussems raia wa Ubelgiji ambaye alitimuliwa mwanzo mwa msimu huu kufuatia kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuipa ubingwa timu hiyo na kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Kocha huyo ameanza kutajwa na mashabiki wa timu hiyo wakiutaka uongozi kumrejesha kwenye timu hiyo baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa, ambapo mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo alitangaza kujiuzulu kabla ya kutangaza kurejea tena.

Aussems alisema kuwa kwa upande wake haoni jambo la kushangaza kwa yanayoendelea kwenye timu hiyo kwa kuwa wanavuna walichokipanda nyuma na wala hakifirii kukubali kurejea kutokana na alichofanyiwa awali.

“Siyo jambo zuri kutaka kujua nini wanachokutana nacho Simba kwa sababu kwangu sioni kama kuna kitu kipya ambacho naweza kusema kwa kuwa wanavuna walichopanda wakati naondoka.

“Unajua katika maisha unapata kile ambacho unastahili kupata na siyo unachotaka kupata sasa na wao wamepata wanachostahili, kifupi siwezi kurejea Simba kwa sababu ilishapita naangalia mambo yangu mengi maana ni ngumu kufanya kazi na watu wasiotaka kukubali,” alisema Aussems.
SOMA NA HII  COASTAL UNION YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR