Home Uncategorized COASTAL UNION YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR

COASTAL UNION YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa hesabu zao kwa sasa ni kuelekea mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Juni 20 Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Mgunda amekiongoza kikosi chake Juni 13 kupindua meza kibabe mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa ligi wakati wakilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.

Mgunda amesema:”Vijana wangu wapo tayari kwa mapambano na nina amini utakuwa mchezo mzuri na mgumu kikubwa ni kwamba tunahitaji pointi tatu.”

SOMA NA HII  BEKI YANGA HATA HAELEWI SABABU YA KUTOPEWA NAFASI KIKOSI CHA KWANZA