Home Habari za michezo PAMOJA NA KUTOLEWA AFCON….TAIFA STARS IMEWEKA REKODI HII YA KIBABE CAF…

PAMOJA NA KUTOLEWA AFCON….TAIFA STARS IMEWEKA REKODI HII YA KIBABE CAF…

Habari za Michezo leo

Timu ya Taifa, Taifa Stars, imetupwa nje kwenye michuano ya AFCON 2023, ikiwa na rekodi mbili mpya.

Stars imeondolewa baada ya kutoka suluhu na DR Congo, lakini ikiweka rekodi ya kukusanya pointi mbili kwenye Kundi F, jambo ambalo haikuwahi kwenye fainali mbili huko nyuma.

Hii ilikuwa mara ya tatu Stars inafanikiwa kushiriki michuano hiyo mikubwa Afrika, ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1980, ikafuzu tena 2019.

Katika fainali zilizopita Stars haikuwahi kufikisha pointi mbili, kwani mwaka 1980 ambayo ilishiriki kwa mara ya kwanza, iliambulia moja kwenye kundi lake baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ivory Coast, lakini ikapoteza 3-1 kwa Nigeria, 2-1 dhidi ya Misri.

Katika fainali za pili mwaka 2019, haikuvuna pointi yoyote baada ya kuchapwa na Senegal 2-0, Kenya 3-2 na Algeria 3-0.

Hii ina maana kuwa Stars imekuwa na mwendelezo mzuri kwenye Afcon za mwaka huu, baada ya kuambulia pointi mbili, suluhu dhidi ya DR Congo, sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia na kupoteza 3-0 ilipovaana na Morocco.

Hata hivyo, timu hiyo imeonekana kuwa na safu nzuri ya ulinzi kuliko kipindi kingine kwenye michuano hiyo, baada ya kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara nne tu, tofauti na mwaka 2019 iliporuhusu mabao sita, mwaka 2019 ikichapwa mabao manane, ingawa kwa sasa imefunga mabao machache kuliko 2019, ilipofunga mawili.

SOMA NA HII  MIPANGO MIPYA YA GAMONDI HADHARANI, NABI ATAJWA