Home Habari za michezo MIPANGO MIPYA YA GAMONDI HADHARANI, NABI ATAJWA

MIPANGO MIPYA YA GAMONDI HADHARANI, NABI ATAJWA

WAKATI watu wakiwa wanawaza Yanga ya msimu ujao itakuwaje basi fahamu kuwa kila kitu kimekamilika kwenye mipango mipya chini ya Kocha, Miguel Gamondi raia wa Argentina kuelekea msimu ujao.

Gamondi ambaye amechukuwa mikoba ya kocha Nasreddine Nabi aliyeondoka baada ya mkataba wake kumalizika hivyo Muargentina huyo anakabiliwa na kazi kubwa ya kuhakikisha anafanya zaidi ya ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.

Yanga chini ya Nabi ilibeba mataji yote ya ndani kwa misimu miwili mfululizo huku ikicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tayari Yanga chini ya Gamondi imeshaonekana katika mchezo wa siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi ambapo walicheza dhidi ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini na kushinda bao 1-0 lililofungwa na Kennedy Musonda.

Tayari chanzo cha ndani kutoka Yanga kiKinasema kuwa, Kocha Gamondi amewataka wachezaji wote wanaocheza katika nafasi za kiungo wa ushambuliaji, mawinga wa pembeni kuhakikisha kuwa wanafunga mabao mengi, ili kuacha kumtegemea mshambuliaji mmoja pakee katika kufunga mabao.

“Kocha mazoezini mara nyingi amekuwa akiwasisitiza wachezaji ambao wanacheza kuanzia namba 7,8,10 na 11 wawe na uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi, anataka msimu ujao kila mchezaji wa mbele afunge mabao ya kutosha ili kumfanya namba 9 asiwe na mzigo mkubwa pekee wa kufunga.

“Ambacho kinaonekana ni kwamba hataki siku ikitokea mshambuliaji wa kati amebanwa basi timu ishindwe kupata mabao, akina Aziz Ki, Pacome Zouzoua na Maxi Mpia ambao wamekuwa wakicheza katika nafasi hizo wamekuwa wakisisitiziwa juu ya kufunga mabao ya kutosha kuanzia mazoezini,” kilisema chanzo hiko.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe akizungumzia maandalizi ya kikosi hicho alisema: “Yanga ya msimu ujao tumemuachia kocha wetu Gamondi yeye ndiye anafahamu kila kitu, ni kocha mkubwa na tumemuamini hivyo tunatarajia kuwa na Yanga bora.”

SOMA NA HII  YANGA WAANZA VISIGIZIO MAPEMA