Kocha Mkuu wa Burundi ‘Intamba Mu Rugamba’, Etienne Ndayiragije amemwaacha nje ya kikosi kiungo wa Simba SC, Saido Ntibazonkiza wakati Burundi ikijiandaa kukabiliana na Namibia kwenye michezo ya kufuzu Afcon 2023 nchini Ivory Coast mwezi ujao.
Saido anatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu baada ya kukataa kushiriki mchezo wa kirafiki dhidi ya Indonesia mapema mwezi Machi mwaka huu.
Mlinda mlango wa Coastal Union Justin Ndikumana ameitwa.