Home Habari za michezo MHOLANZI WA USAJILI SIMBA AANZA NA KIFAA HIKI ….TRY AGAIN AMPA RUNGU...

MHOLANZI WA USAJILI SIMBA AANZA NA KIFAA HIKI ….TRY AGAIN AMPA RUNGU LA KUSHUSHA VIFAA …

Habari za Simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amefunguka kuwa Mkuu wa Kitengo chao cha Skauti, Mholanzi Mels Daalder ana kibarua kigumu cha kufanya maboresho ya kikosi cha timu hiyo, katika kuelekea dirisha kubwa la .

Kauli hiyo ameitoa ikiwa saa chache tangu Mholanzi huyo atangazwe kuwa Mkuu wa Kitengo cha Skauti cha Simba.

Simba imepanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi chao katika msimu ujao baada ya huu kuukosa mataji mawili ya ndani Ligi Kuu Bara na Kombe la FA huku wakiishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hiyo, imepanga kuingiza maingizo mapya zaidi ya nane katika dirisha kubwa la usajili huku ikielezwa kuacha wachezaji wake zaidi ya saba, ambapo miongoni mwa wachezaji ambao wanatakiwa na klabu hiyo yupo kiungo mkabaji, Gatoch Panom Yiech wa St George ya Ethiopia sambamba winga Erick Kabwe wa AS Vita na Leandre Onana wa Rayon Sports.

Akizungumza nasi, Try Again alisema kuwa ujio wa Daalder ni mwanzo wa mikakati yao madhubuti katika maboresho ya kikosi chao kipya.

Try Again alisema kuwa anaamini ujio wake utaleta wachezaji wenye hadhi, ubora na uzoefu wa kucheza michezo ya kimataifa kuelekea msimu uajo wakienda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kutangazwa kwa Daalder kuwa Mkuu wa Kitengo cha Skauti ni mwanzo wa mikakati yao madhubuti katika maboresho ya kikosi chetu cha Simba kuelekea usajili wa dirisha kubwa.

“Huu ni mwanzo tu, tumejipanga kufanya maboresho makubwa ya timu yetu, hili hatutafanya kwenye usajili pekee.

“Tumepanga kuimarisha kila idara kwa kuweka watu ambao tunaamini wataweza kutusaidia kufanya mambo sahihi kwa kulingana na mahitaji ya timu yetu,” alisema Try Again.

SOMA NA HII  RASM...KISA YACOUBA...AIDHA KISINDA AU MAKAMBO MMOJA LAZIMA ASEPE YANGA..ISHU IKO HIVI...

1 COMMENT

  1. Oky fine 🦁💪🇹🇿but we need more “action “than “politics” because on backup to two season we much use politics in registered professional player that offer us profit,but all in all “Not all Gilliters are Gold” we much forgotten privious though we think to the next sezon @2023-2024

    * Remember* ✍️✍️”Too much Democracy is Democrazy'”

    🦁🇹🇿💪 Am loving this team till am dying within this time🦁🇹🇿💪

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here