Home news ZA NDANI KABISA…..MORRISON ‘AIDINDIA’ SIMBA…AKATAA ‘KUMWANGUKIA BARBARA’…SIMBA WANYOOSHA MIKONO…

ZA NDANI KABISA…..MORRISON ‘AIDINDIA’ SIMBA…AKATAA ‘KUMWANGUKIA BARBARA’…SIMBA WANYOOSHA MIKONO…


HABARI kutoka kwa watu wa karibu wa nyota Benard Morrison  wamesema kuwa winga huyo amegoma kuandika maelezo kwenda kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba kuhusu tuhuma za kinidhamu anazotuhumiwa na klabu hiyo.

Morrison raia wa Ghana anadai kuwa yeye hana kosa hawezi kuandika maelezo yoyote wakati huo wazee wa klabu ya Simba SC wameutaka uongozi wa klabu hiyo kuachana na Morrison haraka iwezekanavyo.

Aidha, Klabu ya Simba imethibitisha kutopokea barua ya maelezo kutoka kwa Morrison ambaye wamemsimamisha kwa makosa ya utovu wa nidhamu, Februari 4, 2022. ambapo klabu ya Simba ilitoa taarifa ya kumsimamisha mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa Ofisa wa idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema klabu bado haijapokea maelezo kutoka kwa mchezaji wao Bernard Morrison. Mchezaji huyo anapaswa kuandika barua ya maelezo kwenda kwa mtendaji mkuu.

SOMA NA HII  IMEVUJAAA....HII HAPA 'LIST' YA MASTAA WAPYA SIMBA....WATAANZA KUSHUSHWA MMOJA MMOJA...