Home Habari za michezo IMEVUJAAA….HII HAPA ‘LIST’ YA MASTAA WAPYA SIMBA….WATAANZA KUSHUSHWA MMOJA MMOJA…

IMEVUJAAA….HII HAPA ‘LIST’ YA MASTAA WAPYA SIMBA….WATAANZA KUSHUSHWA MMOJA MMOJA…

Habari za SImba SC

Wakati Simba ikipiga hesabu za itoke vipi kwenye dirisha kubwa la usajili kuweza kurudisha heshima yao, kuna mastaa 12 wanaweza kuja kuvaa uzi wa wekundu hao na kurudisha hadhi ya ubabe wa matokeo kwao.

Tayari Simba kupitia mabosi wake imetamka kwamba itaingia katika rekodi za mashindano ya Afrika ngazi ya klabu na kusaka mastaa wapya ambao watakuja kukiongezea ubora kikosi chao kwa msimu ujao, ambapo hapa ni mastaa waliofanya vizuri kwa rekodi msimu huu unaomalizika

VICTOR SOCHIMA/CHARLES AYAYI

Simba inasaka kipa mpya wa kigeni ambaye atakuja kusaidiana na Aishi Manula baada ya kuondoka kwa Benno Kakolanya lakini hesabu zao zinaweza kutua kwa Victor Sochima wa Rivers United ama Charles Ayayi wa Asec Mimosas

Makipa hawa wawili ambao timu zao ziliishia hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Simba inaweza kuwamudu kumshusha Msimbazi mmoja wao kwa msimu ujao kutoka na rekodi zao bora kwa msimu huu.

Sochima akiwa na Rivers msimu huu amefanya ‘sevu’ 20 huku Ayayi akifanya sevu 11 wakizidiwa Ahmed El Shanawyi wa matajiri wa Pyramids mwenye sevu 31 akiongoza, akifuatiwa na Washington Arubi aliyeichezea msimu huu Marumo Gallants ingawa tayari ameshanyakuliwa na klabu nyingine ya Afrika Kusini huku namba tatu akishika Djogui Diarra wa Yanga.

KOUASSI ATTOHOULA YAO

Simba pia inasaka beki wa kulia hapana shaka wanatakiwa kubaki pale Asec Mimosas wamchukue beki wao wa kulia Kouassi Yao ambaye ameendelea kuwa na msimu bora.

Yao ndiye beki aliyecheza kulia kwenye mechi zote msimu huu anaweza kuja kuwa mbadala au akachuana vizuri na Shomari Kapombe akiwa na ubora wa kujua kupiga krosi za maana lakini pia anaweza kutumia hata kucheza kama winga wa kulia akiwa na kasi akiwa amefanikiwa kutengeneza nafasi kwa asilimia 90:2.1 akizidiwa na winga wa TP Mazembe Philipe Kinzumbi aliyetengeneza nafasi kwa asilimia 90:3.8.

Yao kwa Simba sio mgeni kwao kwani amewahi kukutana nao msimu mmoja uliopita akiwasababishia madhara makubwa katika moja ya bao ambalo wekundu hao walifungwa ugenini na ASEC.

WANLO COULIBALY

Nahodha msaidizi wa Simba Mohamed Hussein Tshabalala ambaye anacheza kama beki wa kushoto naye anaweza kuletewa mtu wa kazi huyu Wanlo Coulibaly kutoka pale timu ya vipaji ASEC.

Hakuna sababu kubwa ya kumuelezea Wanlo kwa kuwa tayari Simba imeshatua kwake wakifanya naye mazungumzo yakiwa yanakwenda vizuri wakijua kwamba jamaa ana ubora wa kucheza kama beki wa kati.

OUSMANE OUTTARA/TSHEPO GUMEDE/FRANCK ZOUZOU/

Mabeki wa kati wawili ambao Simba ikipiga hesabu vizuri mmoja wao anawez akuja kuwafanyia kazi vizuri kwenye ukuta wao akisaidiana na mtu wa kazi Henock Inonga.

Ousmane Outtara ndiye aliyefanya vizuri kuliko wote akiichezea US Monastir ya Tunisia ambao waliishia hatua ya robo fainali wakitolewa na ASEC, msimu huu amefanikiwa kuongoza kwa kuokoa mara 35 akizidiwa na Adam Alliet wa mabingwa wa shirikisho USM Alger aliyeokoa mara 48 huku wa pili akiwa Ali Gabr wa Pyramids aliyeokoa mara 45.

Nyuma ya Outtara yumo Tshepo Gumede aliyeichezea Marumo Gallants ambaye ameokoa mashambulizi makali mara 26 huku Franck Zouzou akiokoa mara 23, Simba inaweza kuchukua mmoja wao na kuja kuimarisha ukuta wao.

MORRICE CHUKWU

Wekundu hao pia wanasaka kiungo wa kati mkabaji hapana shaka kama doria yao itatua kwa mtu wa kazi Morrice Chukwu aliyeichezea Rivers United ambaye licha ya ubora wake mkubwa katika kukaba amekuwa na kazi nyingine bora ya kupiga pasi ndefu zinazofika kwa asilimia 62.5.

KIZUMBI/EMMANUEL LOBOTA/LESIBA NKU

Mawinga watatu hawa wenye kasi ambao wanaweza kuja kuimarisha falsafa za soka la kocha Mbrazil Robert Olivieira ‘Robertinho ambao wameonyesha uwezo mkubwa msimu huu.

Lobota winga wa kulia anaichezea FC Lupopo ya DR Congo ambayo iliishia hatua ya makundi kama ambavyo iliishia Mazembe anayoichezea Kizumbi ambaye ni winga anayetumia vizuri mguu wa kushoto hawa wote wanaweza kuja kuongeza nguvu katika kikosi cha Simba sambamba na Emmanuel Lobota alifika mpaka nusu fainali ya kombe la Shirikisho akiwa na Marumo Gallants.

PAUL ACQUAH

Kinara wa mabao kombe la Shirikisho ni mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ambaye alifunga mabao 7 lakini nyuma yake yupo Mghana Paul Acquah aliyeichezea Rivers ya Nigeria rekodi yake inamtosha kuja kuvaa uzi mweupe na mwekundu hapa nchini akiwa pia ana ubora wa kucheza kama kiungo mshambuliaji yaani namba 10.

SOMA NA HII  SIMBA: HAKUNA ATAKAYETUZUIA KUSEPA NA UBINGWA WA LIGI KUU BARA