Home Simba SC HATMA YA MKUDE NDANI YA SIMBA SC KUJULIKANA JUMAMOSI

HATMA YA MKUDE NDANI YA SIMBA SC KUJULIKANA JUMAMOSI


BAADA ya kuwepo taarifa za chini chini za kusimamishwa kwa kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude kutokana na utovu wa nidhamu, Soka la Bongo linakuja na taarifa za kina, faili la nyota huyo lipo kwenye Kamati ya Maadili na Nidhamu.

Kamati hiyo ipo chini ya Kamanda Kova aliyekuwa Kamanda wa Polisi nchini miaka ya nyuma na kesi yake ilipelekwa na viongozi na wameanza kusikiliza.

Habari za ndani zinadai mchezaji Mkude ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu pia huenda asicheze tena mechi za Ligi Kuu zilizobaki na hivyo akaonekana msimu ujao.

Lakini Kova emenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti kwamba kamati yake itakutana tena Juni 5 (Jumamosi) kwa ajili ya kuendelea kusikiliza shauri hilo na ikiwezekana watamaliza na kulitolea hukumu.

Kamanda Kova aliwajuza wadau na mashabiki wa Simba ambao walikuwa wanasikia tetesi kuhusiana na kusimamishwa kwa staa huyo;

“Ni kweli jambo hilo lipo mezani kwetu na tumeanza kulifanyia kazi, Jumamosi ya Juni 5 hukumu yake itatoka,” alisema.

Wakati Mkude anasubiria hukumu yake, kocha wa timu hiyo, Didier Gomes hajaambatana naye kwenda kuikabili Ruvu Shooting, watakayocheza nayo kesho Alhamisi Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Hiyo sio mara ya kwanza kwa Mkude kusimamishwa na klabu yake akihusishwa na utovu wa nidhamu, aliwahi kukosa kucheza michuano ya Simba walioipa jina la Simba Super Cup na Kombe la Mapinduzi.

SOMA NA HII  BAADA YA ONYANGO KUUNGANA NA WENZAKE LEO...MGUNDA ASHINDWA KUJIZUIA...AANIKA MSIMAMO WAKE...