Home Simba SC CHIKWENDE MATUMAINI YOTE SIMBA

CHIKWENDE MATUMAINI YOTE SIMBA

 PERFECT Chikwende,  kiungo wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes amesema kuwa ana imani ya kufanya vema ndani ya kikosi hicho. 

Imekuwa ikitajwa nyota huyo anaweza kuvunjiwa mkataba wake kutokana na mabosi wa timu hiyo kutomuelewa.

Tayari kiungo aliyechukua namba yake zama zile Francis Kahata mkataba wake umeisha na hakuna mpango wa kumuongezea dili jipya Kahata kwa sasa.

Chikwende ambaye yupo na timu Mwanza kesho huenda akawa sehemu ya kikosi kitakachoanza dhidi ya Ruvu Shooting hajawa na mwendo mzuri ndani ya kikosi hicho akiwa ametoa pasi moja tu ya bao.

Nyota huyo amesema:”Bado mapambano yanaendelea ila imani ni kwamba kwa mechi zijazo tutafanya vizuri na kupata matokeo zaidi,” .

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MKUDE KUTEMWA SIMBA...MBRAZILI AKATA MZIZI WA FITINA...AANIKA MATATIZO YAKE...