Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA MAZEMBE… MORRISON AVUNJA UKIMYA…AIBUKA NA HILI JIPYA YANGA….

KUELEKEA MECHI NA MAZEMBE… MORRISON AVUNJA UKIMYA…AIBUKA NA HILI JIPYA YANGA….

Habari za Yanga

Kiungo fundi wa Yanga, Bernard Morrison ameamua kufunguka kuhusu afya yake huku akiwatoa hofu wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kufuatia kuumia kwake na kukaa nje kwa miezi miwili akipatiwa matibabu.

Raia huyo wa Ghana ambaye anasumbuliwa na nyama za paja amesema hayo kufuatia kuibuka kwa maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa timu yake wakidai kuwa haumwi bali kuna kitu kimefichwa na uongozi juu yake huku wakimtaka aitumikie timu yake inayomhitaji zaidi hasa katika kipindi hiki cha michuano ya CAF.

“Nafahamu wapenzi na mashabiki wa Yanga mlitamani niwepo kikosini kuisaidia klabu yangu hasa katika michuano hii ya Kimataifa ya CAF, lakini mipango ya Mungu ndiyo huanua kila jambo.

“Wengi wanajiuliza nimeumia lini na wapi na kwenye mechi gani, ukweli ni kwamba haya majeraha sio ya leo wala jana. Haya ni majeraha ya muda mrefu na yamekuwa yakinisumbua lakini najitahidi hivyo hivyo, sasa imefika wakati nikaona ni vyrma nikafuata taratibu nzuri za kupata matibabu sahihi, ndiyo maana klabu ikaamua nikatibiwe ili nipone.

“Hii ndiyo sababu kubwa ya kukaa nje kwa muda mrefu kidogo lakini ninaamini nitapona na nitarejea tena uwanjani kuwapa furaha Wananchi. Nipo pamoja na kikosi kuwasapoti na kuwaombea ili tushinde michezo yetu na tusonge mbele katika hatua inayofuata ya kombe la Shirikisho Afrika,” amesema Morrison.

Morrison tangu amejiunga na Yanga msimu huu wa mwaka 2022/23 akirejea kutoka Simba Sc ameitumikia katika michezo 9 ya ligi akicheza dakika 450, akifunga mabao mawili na kutoa pasi za mwisho 2.

Leo Jumapili, Februari 19, 2023 Yanga watakuwa Dimbani katika Uwanja wa Mkapa kuavaana na timu ya TP Mazembe ya Congo DR katika mchezo wa mkondo wa pili wa kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Ikumbukwe kuwa, mechi ya kwanza Yanga alifungwa bao 2-0 na Monastir ya Tunisia wakati TP Mazembe alishinda bao 3-1 dhidi ya Real Bamako ya Mali.

SOMA NA HII  GEITA GOLD KUZIACHA KWENYE MATAA SIMBA NA YANGA...DIMBA LAO KUWA LA KISASA ZAIDI.....