Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUBONDWA JUZI…JEMEDARI SAIDI KAIBUKA NA HILI JIPYA AISEE…AMTAJA AZIZI...

BAADA YA YANGA KUBONDWA JUZI…JEMEDARI SAIDI KAIBUKA NA HILI JIPYA AISEE…AMTAJA AZIZI KI..

Habari za Yanga

Ameandika Mchambuzi Nguli wa Michezo Jemedari Said Kazumari; “Yanga bado wana nafasi kwenye mchezo ujao. Dhahiri kwamba wamejitia ugumu kukubali kichapo cha nyumbani cha mabao 2-1 lakini fainali ni dakika 180, dakika 90 za mwanzo zimeisha USM Algers wanaongoza.

“Kwenye soka mchezaji baada ya kusajiliwa kwa kawaida huwa kuna kipindi cha kuzoea mambo mengi kwenye timu yake mpya hiki kipindi kitaalamu tunaita “Adaptation Period”.

“Nyota ghali kupita wote nchini Stephan Aziz Ki yuko kwenye hicho kipindi kuna mambo anayazoea bado. Si kweli kwamba Aziz Ki ni mchezaji mbaya kama anavyozungumzwa huko kote alikotoka na mpaka Yanga wanamfanya kuwa ghali kupita wengine sio kwakuwa ni mchezaji mbaya, hapana, amefika hapo kwa ubora.

“Tusimhukumu mapema sana klabu na Viongozi wana jukumu la kumsaidia kuonyesha ubora wake ule uliomfanya kuwa ghali.

“Shida ya viongozi wetu ni zao la ushabiki kuna wakati wanafanya mambo kishabiki, tufanye mambo kama Viongozi na tuwaachie mashabiki yale ya kishabiki. Mahaba ya kupitiliza ni kwa mashabiki hatakama kiongozi unayo jaribu kujizuia. Tunaposema huwa hatumchukii yeyote bali kujaribu kujenga tu.

“Imani yangu ni kubwa kwa Aziz Ki kwamba ipo siku atatuziba midomo. Didier Drogba msimu wake wa kwanza Chelsea usingesema ni mchezaji ambaye angekuwa gwiji wa soka akiwa ameacha alama kubwa. Ila alivumiliwa na Viongozi na mashabiki lakini imani ya Jose Mourinho pia, msimu ule alikuwa kwenye ‘adaptation period’ kama anachopitia Aziz.

“Dogo Azizi Ki alikuja kama Mfalme akaanza kuishi Kifalme hata akikosea tunalazimika kurekebisha sisi kwenye maandishi na vipaza sauti na sio kusema ukweli Kama ulivyo waliomkosoa wakaonekana hamnazo na wenye chuki ‘Hatters’ . Bin Kazumari (The voice of the voiceless)”.

SOMA NA HII  RASMI..ADEBAYOR KUTUA SIMBA...MO DEWJI APEWA FAILI LAKE...THAMANI YAKE NI 468 MILIONI..TYR AGAIN AFUNGUKA..