Home Habari za michezo BAADA YA KUWAGAGADUA WYDAD JANA….BENCHIKHA KATAZAMA MASTAA WAKE..KISHA AKASENA HAYA..

BAADA YA KUWAGAGADUA WYDAD JANA….BENCHIKHA KATAZAMA MASTAA WAKE..KISHA AKASENA HAYA..

Habari za Simba

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kudai kuwa bado hawajamalizia kazi kwa kuwa wanakibarua kingine cha mechi mbili ambazo ni muhimu kupata ushindi.

Amesema anaimani kubwa na kikosi chake kinauwezo wa kufanya vizuri na matarajio yake makubwa kuona Simba inasonga mbele kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imebakiza mechi mbili ambapo itasafiri hadi Ivory Coast kucheza dhidi ya Asec Mimosas na baadae watamaliza mechi ya mwisho ya kundi B uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana .

Simba ikipanda hadi nafasi ya pili katika kundi hilo wakiwa na alama tano, Benchikha amesema mechi ilikuwa ya ushindani kila timu ilicheza vizuri na anawapongeza wachezaji wake kufuata maelekezo aliyowapa kwenye uwanja wa mazoezi.

Amesema walipambana na kufanikiwa kupata ushindi katika kipindi cha kwanza jambo ambalo amefanikiwa na kutoruhusu wapinzani kufika katika eneo lao na kuwapa nafasi ya kufunga.

“Wachezaji wamefanya kazi nzuri tumefanya mashambulizi na kufunga lakini hatukuweza kuruhusu bao, kipindi cha pili Wydad walitawala eneo letu walifanya mashambulizi na kubadilisha mfumo kwa kuongeza mabeki .

Nafasi ya kwenda robo fainali ipo wazi, kazi iliyopo kwetu kujiandaa na michezo miwili iliyosalia ambayo tunahitaji ushindi ili kujihakikishia safari yetu ya kucheza robo fainali,” alisema Benchikha.

Ameongeza kuwa baada ya mechi hiyo wanarejea uwanja wa mazoezi kwa ajili ya kufanyia kazi makosa yaliyojitokeza kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu didi ya KMC FC.

Kwa upande wa wachezaji wa Simba akiwemo Willy Essomba Onana ambaye alikuwa shujaa wa mchezo jana, Amesema Kocha Benchikha amempa morali na ari ya kujituma kufanya vizuri kutokana na kumuamini.

Amesema ameonyesha kuwa anaimani naye kitu ambacho kimemuongezea ari ya kujituma huku akiwaahidi mashabiki mambo mazuri zaidi yanayokuja kutoka ndani ya kikosi cha timu yao.

“Huu ushindi ni wetu wote, niwapongeze wachezaji wenzangu tumepambana kitu muhimu kwetu, lakini pia mashabiki wa Simba wanatakiwa kuwa wa kweli, tunapokuwa katika wakati mgumu na furaha tuungane pamoja,” Amesema Onana.

Ameongeza kuwa bado wananafasi ya kuchdza robo fainali kwa sababu wana mechi mbili ugenini na myumbani wanauwezo wa kupata alama muhimu na kufikia kile kinachotarajiwa.

Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein qmesema ilikuwa mechi ngumu walipambana kwa kufuata maelekezo ya kocha na kufanikiwa kupata ushindi nyumbani.

Amesema kazi bado haijamalizika kwa sababu wana fainali mbili mbele yao ya kushinda mechi ya ugenini dhidi ya Asec Mimosas na nyumbani na Jwaneng Gallaxy.

“Tunaenda kupambana, kama tulivyotoka jasho hapa nyumbani basi mechi hizo mbili ninaimani tutajituma na kufanya vizuri, kwa sasa tunasahau hayo matokeo na tunarudi uwanja wa mazoezi na kocha kusahihisha makosa yetu kwa ajili ya mechi ijayo ya ligi,” amesema Mohammed.

Baada ya mechi ya juzi wachezaji wa Simba walipewa mapumziko ya siku mmoja na kujiunga kambini leo kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya KMC FC utakaochezwa jumamosi ya wiki hii, Azam Complex uliopo Chamazi Dar-es-Salaam saa 10:00 jioni.

SOMA NA HII  INJIA HERSI AFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA CEO MPYA..."YALIKUWA MALENGO YETU"...