Home Habari za michezo INJIA HERSI AFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA CEO MPYA…”YALIKUWA MALENGO YETU”…

INJIA HERSI AFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA CEO MPYA…”YALIKUWA MALENGO YETU”…

Habari za Yanga leo

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema amemtuma Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Andre Mtine nchini Misri kwa ajili ya kushiriki katika usimamizi wa upangaji makundi wa michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Ikumbukwe kuwa, Yanga imetinga hatua ya Makundi ya kombe hilo baada ya kuiondoa Club Africain ya Sudan huku Simba ikitinga hatua ya Makundi ya Kombe la Mabingwa Barani Afrika kwas kiuwafunga De Agosto ya Angola.

“Nimemtuma Egypt (CEO) wa klabu yetu, Andre Mtine kwa ajili ya usimamizi wa haki za upangaji wa makundi (CAF)”

“Yalikuwa malengo yetu kuingia hatua hii ya group stage, lakini kuingia hapa ni kwenye hatua nyingine ngumu kwa sababu timu zilizoingia hapa ni timu bora”

“Lakini pia tumepanga kuboresha kikosi chetu kwenye dirisha dogo la usajili kwa ajili ya kupandisha thamani ya kikosi chetu Kuelekea kwenye michuano ya (CAF),” Eng. Hersi Said.

SOMA NA HII  SHABIKI SIMBA:- TUTAMUUNGA MKONO INONGA ILA SIO KUPAKA MKOROGO NA KUJA NAO UWANJANI..