Home Habari za michezo SHABIKI SIMBA:- TUTAMUUNGA MKONO INONGA ILA SIO KUPAKA MKOROGO NA KUJA NAO...

SHABIKI SIMBA:- TUTAMUUNGA MKONO INONGA ILA SIO KUPAKA MKOROGO NA KUJA NAO UWANJANI..

Habari za Simba leo

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo watamsapoti beki wao Henock Inonga ambaye ametajwa kuwa ‘mgeni rasmi’ kwenye mchezo wao dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Mchome amesema hayo baada ya Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kutangaza kuwa, Jumamosi itakuwa simu maalum ya Inonga kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng utakaopigwa katika Dimba la Mkapa.

β€œIshu ya mgeni rasmi, msemaji alikuja na staili ya makoti (Mgeni rasmi Kibu Denis) tukaenda kula chuma 5 kama tumesimama (mechi ya Yanga), tukaja mgeni rasmi Robertinho tukala chuma moja, leo anakuja na mgeni rasmi Inonga, staili zake imeshindikana kwenda nazo kwa sababu staili za Inonga kwa Tanzania ni haramu.

β€œStaili ya mkorogo, kichupa, kitaulo, umwambie mwanaume wa Dar ajichubue ni matusi. Sisi tutamsapoti mgeni rasmi Inonga kwa sababu inamheshimisha mchezaji lakini staili zako hatukuigi babu, hizo ni za kwako na Wakongo wenzako huko.

β€œIshu ya kuhamasiha kwa kutumia wachezaji, Yanga ndiyo wameanzisha, sisi Simba tumekopi, sio vibaya kukopi jambo zuri kwa sababu hata wao wamekopi Yanga Day kutoka Simba Day. Maendeleo hayana chama, ukiona mtu anafanya jambo jema, ruksa kuiga,” amesema Mchome.

SOMA NA HII  KUMBE ILE ISHU YA BILIONEA WA CHELSEA KUPEWA SUMU AKIWA UKRAINE IKO HIVI AISEE....

1 COMMENT