Wiki imeanza vyema zaidi kwa Klabu ya soka ya KMC, ambao wamepata mdhamini mpya, ikiwa ni neema kwa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania. KMC wameingia rasmi mkataba wa udhamini na klabu ya Meridianbet, ambao ni mabingwa na Kampuni ya kwanza ya ubashiri Tanzania.
KMC imekuwa ni klabu inayokua kwa kasi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014, ikiwa haijawahi kushuka daraja tangu ipande ligi kuu. Ni timu inayoonesha uwezo, katika kusalia kwenye ubora wa Ligi kuu Tanzania, moja ya Ligi zenye ushindani mkubwa sana barani Afrika kwa zaidi ya miaka 7.
“Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi, kwa kuwa sisi ni bora, ubora wetu umetuletea mdhamini mwingine ambaye ni Meridianbet. Tunamtambulisha kwenu Meridianbet kuwa mdhamini wetu mkuu kwa miaka mitatu.”
Meridianbetwanabainisha kuwa wataendelea kujihusisha zaidi na michezo, na wanatazamia kuona mafanikio makubwa na klabu ya KMC ndani ya miaka ijayo.
“Kama kampuni tunatazamina kuona klabu hii ya KMC inafanikiwa na tutaendelea kuwa bega kwa bega kuhakikisha tunafanikiwa pamoja. Tunajivunia kuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya soka linapokua na kutoa fursa mbali mbali za kiuchumi na kuwaleta watu pamoja.” – Twaha Mohamed, Afisa Masoko wa Meridianbet.
Meridianbetni mabingwa wa ubashiri, wakiwa na maduka mengi nchini Tanzania, na kuongoza kwa ubashiri wa mtandaoni kwa michezo yote pendwa na kasino ya mtandaoni.Ubashiri wa Meridianbet pia unaweza kufanyika kwa USSD kwa kupiga *149*10#