Home Habari za michezo YANGA HAKUJAPOA….KAZE ALIAMSHA TENA KUELEKEA MECHI YA KESHO NA SINGIDA…

YANGA HAKUJAPOA….KAZE ALIAMSHA TENA KUELEKEA MECHI YA KESHO NA SINGIDA…

Kikosi cha Yanga SC

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze  amesema pamoja na uchovu waliokuwa nao wachezaji wao na ratiba kuwabana lakini wamejipanga kuhakikisha kesho Alhamisi wachukua pointi tatu dhidi ya Singida Big Stars.

Akizungumza, kocha huyo amesema kikosi chao kimeingia kambini  Avic Town Kigamboni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wanajua utakuwa mgumu kutokana na ubora wa kikosi cha wapinzani wao lakini lengo lao ni kuzibakisha Jangwani pointi zote tatu.

“Nimchezo mgumu sababu ratiba imekuwa ngumu kwetu tumekuwa tukicheza mechi kila baada ya siku mbili lakini haina namna lazima tucheze na lazima tushinde kwanza tunataka pointi tatu lakini jambo la pili ni kuhakikisha tunailinda rekodi yetu ya kutopoteza mchezo kwenye ligi,” amesema Kaze.

Kocha huyo amesema leo asubuhi wamefanya mazoezi ya Gym na jioni watafanya mazoezi ya uwanjani na kesho watafanya mazoezi kwa awamu moja pekee ya asubuhi kwa ajili ya kuuandaa mwili kabla ya mchezo huo siku ya Alhamisi.

SOMA NA HII  PABLO ALIAMSHA HUKO...AKATAA KUPOKEA BARUA YA KUVUNJA MKATABA...ADAI HAKUPANGA KUONDOKA SIMBA MAPEMA...