Home Uncategorized MWADUI FC: TUPO TAYARI KUSAKA POINTI TATU ZA SIMBA

MWADUI FC: TUPO TAYARI KUSAKA POINTI TATU ZA SIMBA

 


KHALID Adam, Kocha Mkuu wa Mwadui FC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wao wa kesho, Oktoba 31 dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.


Akizungumza na Saleh Jembe, Adam amesema kuwa wanaitambua vema Simba kwa kuwa wamekutana nao mara nyingi uwanjani jambo ambalo linamfanya aamini kwamba watapambana kusaka ushindi.


“Tumetoka kupoteza mchezo wetu uliopita imetuumiza ila nimewaambia wachezaji kwamba wasiwe na presha yaliyopita ni muhimu kusahau na kutazama mechi zetu zijazo.


“Mchezo wetu dhidi ya Simba ni muhimu kwetu kupata ushindi ili turejeshe hali ya kujiamini na hilo linawezekana ikiwa kila mchezaji atajituma na kusaka matokeo kwa juhudi.


“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao na kuona namna ambavyo tutafanya, tupo tayari kwa ushindani,” amesema.


Timu zote mbili mechi zao za mwisho kwa msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara zimepoteza kwa kuyeyusha pointi tatu.


Mwadui FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 6-1 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mwadui Complex na Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru.


Kumbukumbu yao msimu uliopita mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza ilikuwa mbele ya Mwadui FC ambapo ilifungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Gerald Mdamu ambaye kwa sasa yupo ndani ya Klabu ya Biashara United. 

SOMA NA HII  SABABU YA RUVU SHOOTING KUFANYA KLINIKI KWA WACHEZAJI YATAJWA