Home Yanga SC YANGA KAMILI KULITWAA TAJI LA SIMBA, KIGOMA

YANGA KAMILI KULITWAA TAJI LA SIMBA, KIGOMA


 UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba unahitaji kutwaa Kombe la Shirikisho ambalo lipo mikononi mwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Yanga ikiwa imemaliza ligi nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zake 74 itakutana na Simba Julai 25 kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho na Simba ni mabingwa wa ligi wakiwa na pointi 83.


Pia Simba ni mabingwa watetezi wa taji hilo baada ya kulitwaa msimu uliopita walipocheza fainali na Namungo FC ya Lindi, Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga amesema kuwa wanatambua kwamba mchezo wao ujao utakuwa mgumu lakini wanahitaji ushindi ili kutwaa Kombe la Shirikisho.


“Tunatambua kwamba tutakutana na Simba kwenye mchezo wa fainali Kigoma, hatuna mashaka tupo tayari na tunahitaji ushindi ili kutwaa taji hilo kwani ni mpango wetu kushinda.


“Hakuna namna ambayo itatufanya tuweze kutwaa taji hilo zaidi ni kucheza vizuri na kupata ushindi hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.

Timu zote mbili kwa sasa zipo Kigoma kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao umevuta hisia za wengi ikiwa ni pamoja na wakazi wa mwisho wa reli, Kigoma.

SOMA NA HII  DIAMOND 'KUKINUKISHA' SHEREHE ZA YANGA LEO....KALIPWA MAMILIONI HAYA KWA TUKIO HILO TU..