Home Uncategorized BREAKING:YANGA YAMFUTA KAZI KOCHA MSERBIA ZLATKO

BREAKING:YANGA YAMFUTA KAZI KOCHA MSERBIA ZLATKO

 


UONGOZI  wa Klabu ya Yanga leo Oktoba 3,2020 umefikia makubaliano ya kumfuta kazi kocha wao mkuu, Zlatko Krmpotic raia wa Serbia aliyechukua mikoba ya Luc Eymael.


Zlatko amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara ambapo katika mechi hizo ameshinda mechi nne na kulazimisha sare moja ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons.

Leo Oktoba 3 amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Coastal Union ambapo Yanga ilishinda mabao 3-0.


Taarifa rasmi iliyotolewa na Klabu ya Yanga imeeleza kuwa wamefikia makubaliano ya kusitisha makubaliano kwa pande zote mbili.


SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII