Home Simba SC MORRISON WA KIGOMA BEGA KWA BEGA NA MZEE DALALI, MCHETUAJI AMWAMBIA AKASOME

MORRISON WA KIGOMA BEGA KWA BEGA NA MZEE DALALI, MCHETUAJI AMWAMBIA AKASOME

 MZEE Hassan Dalali amesema kuwa miongoni mwa mashabiki ambao wanaompenda pia ni pamoja na Bernard Morrison wa Kigoma.

Morrison huyo alipata pia bahati ya kuonana na mchetuaji mwenyewe Morrison ambapo alimwambia jambo la msingi ambalo anapaswa kulifanya ni kwenda shule.

Sababu kubwa ya kumwambia hivi ni pale ambapo walikuwa hawaelewani lugha kwa kuwa Morrison alikuwa anaongea Kiingereza jambo lililokuwa linampa tabu Morrison wa Kigoma.

Morrison alimpa zawadi ya jezi yake yenye namba tatu na kumuambia pia baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho waonane.

Kwa upande wa Dalali ambaye ni Mwenyekiti wa zamani wa Simba amesema kuwa yupo pamoja na Morrison wa Kigoma ambaye anampenda pia.


“Morrison wa Kigoma anampemda Dalali, kwetu sisi Simba ni amani na upendo hivyo tunapendana wakati wote,” amesema. 

Kesho Julai 25, Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Yanga ambao nao pia watakuwa wanasaka ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho,  mwisho wa reli Kigoma.


SOMA NA HII  PICHA: TAZAMA JINSI CHAMA ALIVYOTUA BONGO KIJASUSI...APOKELEWA KIMYA KIMYA BILA 'SHAZI'...